13.02.2014

Foreplan herbal clinic hamilton

BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala limevifutia usajili na kusitisha huduma za vituo vitatu vya tiba asili na tiba mbadala nchini ikiwemo Foreplan Clinic ya tabibu Juma Mwaka, Mandai Herbal Clinic ya tabibu Abdallah Mandai pamoja na Fadhaget Sanitarium Clinic ya tabibu Fadhili Kabujanja.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Edmund Kayombo alisema vituo hivyo vimefutiwa usajili na kusitishiwa huduma kutokana na kukiuka masharti ya baraza, ikiwemo urushaji wa matangazo yasiyokuwa na kibali kutoka katika baraza hilo pamoja na baadhi ya waganga kuendelea kutoa elimu ya tiba asili na tiba mbadala kwa umma kinyume cha katazo la waziri mwenye dhamana ya afya.
Licha ya kuvifutia usajili vituo hivyo, pia baraza hilo limetoa adhabu katika vituo mbalimbali ikiwemo Amani Herbal Clinic inayomilikiwa na Esbon Baroshigwa ambaye amepewa barua ya onyo, Ndulu Herbal Clinic inayomilikiwa na Castory Ndulu pia amepewa barua ya onyo.


Huku Sigwa Herbal Clinic inayomilikiwa na Simon Rusigwa amesimamishwa kutoa huduma huduma za tiba asili kwa miezi sita, Lupimo Sanitarium Clinic inayomilikiwa na John Lupimo amesimamishwa kutoa huduma kwa miezi sita. Aidha, Kayombo alisema waganga wote wa tiba mbadala wanatakiwa kuanza uhakiki wa vyeti vya sekondari na vyuoni, hivyo waviandae na kuvifikisha katika baraza hilo ndani ya mwezi mmoja. Alisema kwa mujibu wa sheria mganga kabla ya kupeleka tangazo katika vyombo vya habari ni lazima kwanza tangazo hilo lipitiwe na baraza na kupewa kibali, pia taarifa inayohusu tiba asili na tiba mbadala lazima ipitiwe na baraza kabla ya kufikia umma.


Aliongeza kuwa, hivi karibuni kumekuwepo na baadhi ya matangazo na vipindi vinavyorushwa katika redio, magazeti, runinga na mitandao ya kijamii kuhusu utoaji wa matibabu ya tiba asili na tiba mbadala kinyume cha utaratibu na maadili.Homeopathy treatment for cancer bangalore university
Chinese remedy knee pain treatment
Relieve gas pain with yoga


Comments to «Foreplan herbal clinic hamilton»

  1. Narin_Yagish writes:
    TD exists and advises marketers to make no efficacy claims (Chinese Medicine Centre.
  2. KOMENTATOR writes:
    Vaccine towards the tumor, kick-starting.